Ukiibiwa Mume au Mke wewe nipigie nitashughulika naye - RC Mbeya - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, March 13, 2019

Ukiibiwa Mume au Mke wewe nipigie nitashughulika naye - RC Mbeya


Ukiibiwa Mume au Mke wewe nipigie nitashughulika naye - RC Mbeya

Ukiibiwa Mume au Mke wewe nipigie nitashughulika naye - RC Mbeya
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amesema kuwa kwa wakazi wa Mbeya atakaye ibiwa mke au mume ampigie atashughulika nae muibaji.

"Ukimuona mtu ni mwizi tupigie simu muda wowote na mimi huwa naacha namba yangu ya simu kwenye majukwaa kama haya na leo hii ntaacha namba yangu ya simu, tuma sms muda wowote ila usipige kwasababu siwezi kuwasikiliza Wana - Mbeya wote," alisema Chalamila.

"Wewe tuma sms andika mimi ni mwana Matundasi nimeibiwa mume wangu, maana kuna wamama wengine wanaiba waume, wanaume wengine wanaiba wamama wewe niambie mimi nitashughulika nae," alisisitiza RC Chalamila.

Chalamila ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Matundasi huko Mkoa Mbeya. 
Loading...

No comments: