UMOJA WA MATAIFA WAPINGA PENDEKEZO LA IAAF KUWEKA VIPINGAMIZI KWA BAADHI YA WANARIADHA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, March 27, 2019

UMOJA WA MATAIFA WAPINGA PENDEKEZO LA IAAF KUWEKA VIPINGAMIZI KWA BAADHI YA WANARIADHA


Umoja wa Mataifa umesema mipango ya Shirikisho la Kimataifa la Riadha (IAAF) ya kutaka kuwaweka kwenye kundi maalum baadhi ya wanariadha kutokana na hali zao za kimaumbile kinapingana na haki za binadamu. 

Bingwa wa mbio za mita 800 kutoka Afrika Kusini, Caster Semenya anapambana ili kuzuia hatua inayotaka kuchukuliwa na Shirikisho la Riadha duniani linalotaka kuweka viwango maalum vya vichocheo vya mwilini kwa wakimbiaji wa kike. 

Semenya amekuwa akitajwa kua na kiwango kikubwa cha homoni za kiume hali iliyozua maswali na malalamiko kwa baadhi ya wanariadha wengine wa kike. 

Umoja wa Mataifa umesema mpango huo “hauna ulazima, udhalilishaji na wenye madhara”, hata hivyo IAAF imesema pendekezo lililopelekwa Umoja wa Mataifa lina hoja zisizojitosheleza. 
Loading...

No comments: