UPDATES: Abiria Kutoka nchi 33 Waliosafiri Kwenye Ndege iliyopata Ajali Wamekufa - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, March 11, 2019

UPDATES: Abiria Kutoka nchi 33 Waliosafiri Kwenye Ndege iliyopata Ajali Wamekufa


Taarifa ya Kampuni ya ndege ya Ethiopian Airlines imesema abiria kutoka nchi 33 waliosafiri kwenye ndege iliyopata ajali wote wamekufa.

Kulingana na Msemaji wa Kampuni hiyo Asrat Begashaw Ndege ya kampuni ya Ethiopia aina ya Boeing 737 iliyokuwa ikisafiri kutoka Adis Ababa kuelekea Nairobi imeanguka leo asubuhi.

Taarifa ya Shirika la ndege la Ethiopia- Ethiopian Airlines inasema walipoteza mawasiliano na ndege iliyopata ajali dakika sita baada ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa Adi Ababa.

Takriban wasafiri 149 na wahudumu wanane wanadhaniwa kuwa walikuwemo kwenye ndege hiyo

Kampuni hiyo inasema imeanzisha kituo cha kupata taarifa kuhusu familia na marafiki za watu waliliokuwemo ndani ya ndege hiyo.
Loading...

No comments: