URUSI: BUNGE LAPITISHA SHERIA, WATAKAOIKOSEA HESHIMA SERIKALI MTANDAONI KUKIONA CHA MOTO - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, March 7, 2019

URUSI: BUNGE LAPITISHA SHERIA, WATAKAOIKOSEA HESHIMA SERIKALI MTANDAONI KUKIONA CHA MOTO


Bunge la nchini URUSI kwa pamoja limepitisha mswada wa sheria ya mitandao ya kijamii ambao umedhamiria kudhibiti ukiukwaji wa sheria, utamaduni na heshima kwa serikali, viongozi na taifa kwa ujumla. 

Sheria hiyo iliyotajwa kuwa imejaa utata imeipa mamlaka Mahakama ya kuwafunga wanaoikosea heshima Serikali na viongozi wake kupitia mitandao ya kijamii. 

Sheria hiyo iliyopitishwa na Bunge hilo itamgusa hata atakayemsema vibaya mitandaoni Rais wa nchi hiyo Vladmir Putin.

Katika sheria hiyo kuna kipengele kinachoainisha kuwa yule mkosaji anayerudiarudia kosa hilo atapata ongezeko la adhabu zaidi ya hiyo iliyopangwa kabla.

Mbunge wa Upinzani Sergei Ivanov akipinga sheria hiyo tata, alisema ''Kama tukiacha kumuita mjinga MJINGA, hawezi kuacha Ujinga wake''.

Putin anatarajiwa Kusaini Sheria hiyo wiki chache zijazo. 
Loading...

No comments: