UVCCM Wasema Wamemsamehe Lowassa Baada ya Kukiri Makosa na Kuahidi Kujirekebisha - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, March 12, 2019

UVCCM Wasema Wamemsamehe Lowassa Baada ya Kukiri Makosa na Kuahidi Kujirekebisha


UVCCM Wasema Wamemsamehe Lowassa Baada ya Kukiri Makosa na Kuahidi Kujirekebisha
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) umesema wamesahau na kumsamehe Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa baada ya kukiri makosa na kujirekebisha.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatatu Machi 11, 2019 jijini Dodoma na Mwenyekiti wa umoja huo , Kheri James  wakati wakizungumza na waandishi wa habari kuwa kama akitokea mtu akahoji kwa nini Lowassa amesamehewa na kukubaliwa na CCM anyooshe mkono kwamba yeye hana dhambi.

Amehoji waliobainika kuhusika katika ripoti ya ukaguzi wa mali za CCM kama yupo aliyepelekwa mahakamani kwa makosa na kwamba anayekiri makosa yake na kujirekebisha husamehewa.

Lowassa  alihamia CHADEMA  Julai 28, 2015 lakini  March Mosi, 2019 alitangaza kurejea chama chake cha zamani cha CCM.
Loading...

No comments: