VAN GAAL: "DI MARIA ALISHINDWA KUKABILIANA NA PRESHA YA PREMIER LEAGUE". - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, March 27, 2019

VAN GAAL: "DI MARIA ALISHINDWA KUKABILIANA NA PRESHA YA PREMIER LEAGUE".


Aliyewahi kuwa kocha wa Manchester United Louis Van Gaal amesema kuwa mchezaji Angel Di Maria ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya PSG nchini Ufaransa, alishindwa kufanya vyema enzi hizo akiwa Manchester United kwasababu alishindwa kukabiliana na presha ya Ligi kuu ya Uingereza na si vinginevyo. 

Louis Van Gaal aliyasema hayo akijibu mapigo baada ya kuambiwa na mwandishi wa habari kwamba Angel Di Maria anamlaumu yeye kwamba ndio chanzo cha kushindwa kucheza vizuri katika ligi ya Uingereza. 

Lakini kocha huyo wa kidachi amedai kwamba alimpa Di Maria nafasi ya kucheza kila nafasi katika eneo la ushambuliaji lakini hakucheza vizuri na presha kubwa kutoka kwa wachezaji wa timu pinzani pindi akiwa na mpira ndio alishindwa kuhimili. 
Loading...

No comments: