Vanessa Mdee Apangua Tuhuma za Kutohudhuria Misibani - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, March 12, 2019

Vanessa Mdee Apangua Tuhuma za Kutohudhuria Misibani“Niliona nipotezee lakini naomba niseme once and for all. Misiba na mazishi ni kama ibada, ukishiriki sio habari ya kutangaza kama tamasha. Nimeona watu wanataka kunishikilia bango kama mtu asiyehudhuria au asiyeshiriki katika ibada hizi. 

"Kama unataka kufaham nilikuwepo katika misiba yote ya hivi karibuni lakini sikupenda kutangaza uwepo wangu kutokana na kupitia misiba mizito katika maisha yangu kama watu wengine wengi. 

"Siku ya kesho itakuwa miaka 12 tangu nimpoteze baba yangu mzazi na mwaka huu ni miaka miwili tangu nimpoteze Dada yangu ( mtoto wa kwanza wa baba) i bet you didn’t even know, why? Because I prefer to silently pray for the family and loved ones, I’ve found that only God can bring some relief in these situations. “ameeleza Vanessa Mdee na kufafanua.Itakumbukwa kuwa Tanzania imekumbwa na misiba ya watu maarufu kwenye tasnia ya habari na burudani kwa wiki tatu mfululizo ikiwemo msiba wa Rapper Godzilla, Mtangazaji wa clouds FM, Ephraem Kibonde na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.
Loading...

No comments: