VITU VITATU AMBAVYO TANZANIA INAPASWA KUVIFANYA KUONDOKANA NA UMASIKINI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, March 23, 2019

VITU VITATU AMBAVYO TANZANIA INAPASWA KUVIFANYA KUONDOKANA NA UMASIKINI

VITU VITATU AMBAVYO TANZANIA INAPASWA KUVIFANYA KUONDOKANA NA UMASIKINI Idadi ya watu Tanzania kutokana na takwimu za sensa ya mwaka 2012 ni watu zaidi ya milioni 40, huku ikiwa karibia nusu ya  watu zaidi ya milioni 17  ni masikini. Leo hii Tanzania inakadiriwa kuwa na watu zaidi ya milioni 50, ikiwa ni ya sita kwa kuwa na watu wengi zaidi barani Afrika huku nchi inayoongoza  kwa kuwa na watu wengi zaidi ni Nigeria ikiwa na watu takribani milioni 180. Takwimu zilizofanywa na UNFPA inakadiriwa kuwa ifikapo mwaka 2050 Tanzania itakuwa nchi yenye watu  zaidi milioni 130 na kuwa nchi yenye kuwa na idadi kubwa zaidi barani Afrika. Hii inaashiria nini? Taifa litakuwa na vijana  wengi na mahitaji au huduma za kijamii zitahitajika kwa wingi zaidi. Je hii inamaana gani kwenye sekta mbali mbali? Nchi itahitaji chakula kingi cha kutosheleza kulisha watu zaidi ya milioni 130 ifikapo 2050. Uwekezaji wa kwenye kilimo unaotumia eneo dogo (kwa kutumia teknolojia) na uzalishaji mwingi kwa muda mrefu itaongeza chachu ya maendeleo endelevu na kuondokana na janga la njaa ambapo imezungumziwa kwenye lengo namba 2 la Malengo ya Maendeleo Endelevu au SDGs (Sustainable Development Goals) yaliyowekwa na Umoja wa Mataifa ifikapo mwaka 2030 yawe yametimia. 

Je Vitu gani vya kuvipa kipaumbele ili kuondokana na umaskini huu?

1. Kuwekeza kwenye elimu kwa wasichanaKumwezesha mwanamke ni kuwezesha jamii nzima, zoezi hili la  kumwezesha mtoto wa kike linanza kwa kumpa elimu  kuanzia akiwa mdogo. Kutokana na changamoto za hapa na pale anazopata mtoto wa kike kuna sababu kadha wa kadha zinazomnyima asipate haki ya msingi ya kupata elimu bora. Sababu kama vile mimba za utotoni zinachangia kwa kiasi kikubwa kumnyima msichana haki ya kupata elimu kama mtoto wa kiume, hii inatokana na sababumbali mbali  kama vile kiwango kikubwa cha umasikini, ubakaji, kutokuwa na elimu ya jinsia na afya ya uzazi, malezi mazuri ya wazazi. Pia mazingira magumu/hatarishi yanachangia kumnyima mtoto wa kike kupata elimu.  Mila potofu pia ni kikwazo kwao. 
Je nini kifanyike? Uwekezaji wa elimu kwa watoto wakike itasaidia kuondokana na umasikini na  wategemezi wengi, ukimwezesha mtoto wa kike kupata elimu bora na kufikia malengo yake umewezesha pia na watoto wake ambao ni vijana wanaotegemewa kuongoza nchi na nguvu kazi ya taifa kwa ujumla. Miundombinu mizuri ya elimu kama vile madarasa ya kutosha, teknolojia, nishati safi na nafuu, barabara nzuri na mazingira mazuri ya kufundishia pamoja kujifunzia yatakuwa chachu ya kumwezesha mtoto wa kike kupata elimu bora ambayo itakuwa chachu ya maendeleo. Uboreshaji wa sera ya elimu kulingana na mahitaji ya kila siku itamsaidia pia kumpa nafasi kubwa mtoto wa kike kupata elimu bora na kutengeneza kizazi chenye kujitambua na wenye udhubutu wa kujaribu kwa nia ya kuleta maendeleo katika jamii. 2. Uwekezaji kwenye Afya na Ustawi 

Uwekezaji duni katika huduma za afya unahusishwa na ukuaji wa uchumi, na hivyo kupunguza umasikini. Tanzania inakabiliana na idadi kubwa ya viashiria vya afya vinavyojumuisha malaria, kifua kikuu na vifo vya watoto wachanga na wajawazito, ambayo yote yana athari kubwa ya uzalishaji.

Ili kukomesha umasikini, ni lazima tufanye mgawanyiko wa idadi ya watu kupitia uwekezaji katika afya, elimu na maisha hasa kwa vijana wetu. Katika maneno aliyoifanya mnamo Oktoba 2017, Siku ya Kimataifa ya Kuondokana na Umasikini, Profesa Babatunde Osotimehin aliyekuwa mwakilishi wa zamani wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Idadi ya Watu (UNFPA) - alisema kuwa "wakati miundo ya umri wa nchi inabadilika vizuri, maana yake ina watu wengi umri wa kazi kuliko wategemezi, wanaweza kuona kukuza maendeleo, inayojulikana kama mgawanyiko wa idadi ya watu, ili waweze kuwawezesha, kuelimisha na kuwatumia vijana wao. "

 Nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara - mipaka ya mwisho ya umasikini duniani - inashuhudia ukuaji wa idadi ya watu, na eneo hilo linatarajiwa kukua kwa asilimia 51 kwa kipindi cha miongo mitatu ijayo. 

Ukuaji mdogo wa wakazi wa chini sio sababu ya moja kwa moja kuondokana na  umasikini. Badala yake, idadi ya vijana wenye ujuzi, wenye afya na wenye ujasiri, kama ilivyokuwa nchini China, ni kichocheo bora cha ukuaji. Hata hivyo, ukosefu wa mipango au mgawanyo wa rasilimali haitoshi kwa kuunganisha idadi hii ya watu inaweza kupiga hatua.


3. Kuongeza  fursa za kiuchumi na kutumia teknolojia vizuri. 

Karne hii ya 21 imetawaliwa na teknolojia ya hali ya juu ukilinganisha na miaka ya nyuma, tumeona mabadiliko makubwa kwenye sekta ya teknolojia kuanzia kwenye mitandao ya kijamii, afya, elimu na viwanda. Fursa mbali mbali za kiuchumi zimekuwa zikiletwa na tecknolojia, zimesaidia kwa kiwango kikubwa kutenegneza ajira kwa vijana na kufungua masoko mapya ya biashara. 
Kutokomeza umasikini kutachangiwa na fursa za kiuchumi za kutumia rasilimali watu ambao ni vijana na wanawake kufungua masoko mapya ya ajira kwa kuwekeza kwenye teknolojia. Kama teknolojia itatumika vizuri italeta mabadiliko chanja kwa taifa na kutengeneza ajira zaidi kwa vijana na wanawake kufikia malengo ya maendeleo endelevu.
x
Loading...

No comments: