Vodacom yazindua huduma mpya ya kurahisisha biashara inayoendana na mabadiliko ya kidijitali - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, March 27, 2019

Vodacom yazindua huduma mpya ya kurahisisha biashara inayoendana na mabadiliko ya kidijitali

 Hisham Hendi, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Vodacom, akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitengo maalum kwa ajili ya kushughulikia mahitaji ya wateja wanaofanya biashara kuanzia makampuni madogo-ofisi ndogo za nyumbani(Soho), wafanyabiashara wa kati (SMEs) na makampuni makubwa jana jijini Dar es salaam. 
Hisham Hendi, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Vodacom, na Arjun Dhillon, Mkurugenzi wa Kitengo maalum cha Biashara wakizungumza wakati wa uzinduzi wa kitengo hicho maalum kwa ajili ya kushughulikia mahitaji ya wateja wanaofanya biashara kuanzia makampuni madogo-ofisi ndogo za nyumbani(Soho), wafanyabiashara wa kati (SMEs) na makampuni makubwa jana jijini Dar es salaam. 26th Machi 2019, Dar es Salaam: Katika jitihada za kuhakikisha biashara zinaenda sambamba na mabadiliko ya  masoko ya kisasa, kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania PLC, leo imezindua kitengo kwa ajili ya kushughulikia  huduma zinazoenda sambamba na mahitaji ya wateja wake wanaofanya biashara kuanzia makampuni madogo-Ofisi ndogo za nyumbani (Soho's), Wafanyabiashara  wa kati (SMEs) na Makampuni makubwa.
Lengo kuu la huduma hii ni kuwawezesha kufanya biashara kwa ufanisi zaidi, kuhimili ushindani, kujenga mtandao wa kibiashara na kuwawezesha kupata huduma zote za kurahisha biashara zao bila kuhangaika na masuala yaliyo nje ya biashara zao za msingi.
“Ulimwenguni kote kumetokea mabadiliko ya njia za kufanya biashara kutoka njia za zamani kwenda njia za kidijitali, kutumia mitandao na teknolojia za kisasa kama cloud ,tunatarajia wateja wetu kwenda sambamba na  mabadiliko haya ili kufanya biashara zao kwa ufanisi na kuhimili ushindani katika masoko nasi tunaamini ni wabia wao muhimu katika kuleta ufumbuzi wa kufanikisha biashara zao”, alisema Hisham Hendi, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC.
Makampuni makubwa kama mabenki na sekta ya umma yanatafuta ufumbuzi wa ubunifu ambao utarahisisha shughuli za uendeshaji, kuhimili ushindani na kuhakikisha mali zake ziko salama. Vodacom Tanzania PLC kampuni kinara inayoongoza kutoa huduma za ubunifu wa kidijitali inawezesha kupata huduma za utambuzi wa maeneo, huduma za kompyuta kutumia teknolojia ya kisasa ya Cloud, data MPLS, huduma za simu ambazo mpigaji hatotozwa gharama za kupiga simu na biashara kutumia  M-Pesa ili kuwezesha makampuni makubwa kufanya kazi kwa tija na ufanisi.
Msukumo wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda umepelekea kuanzishwa kwa biashara ndogo na za kati ambazo uendeshaji wake kwa ufanisi unahitaji huduma za ubunifu wa kiteknolojia za kisasa ili kuzipunguzia gharama za uendeshaji
"Vodacom inayo dhamira ya kufanikisha ukuaji wa biashara nchini Tanzania kupitia ubunifu wake wa huduma za teknolojia ya kidijitali za kuwarahisishia wafanyabiashara kufanikisha malengo yao na kujiandaa kwa siku zijazo na ndio maana tumewaletea huduma hizi” alisema Bw, Hendi.
Biashara zenye ukubwa wa kati kama asasi zisizo za Kiserikali (NGO’s) ambazo zimejipanga kuendesha shughuli zake kwa njia za  kisasa na ambazo zinatoa kipaumbele kutumia teknolojia za kisasa yatafaidika na huduma kama IoT (Internet of Things) , SIM Manager na utumaji wa ujumbe wa maneno kwa watu wengi kwa wakati mmoja (bulk SMS).
Kwa upande wa biashara ndogo na Ofisi ndogo za nyumbani (Soho's) zitanufaika kwa kubana matumizi na kujenga mtandao wa biashara kupitia huduma ya M-Pesa, huduma za kurahisisha biashara na utumaji wa ujumbe wa maneno kwa watu wengi kwa pamoja wataweza kubadilisha biashara zao na kuzifanya kukua zaidi.
Kupitia ubunifu huu mkubwa ambao unabadilisha mbinu za kufanya biashara, Vodacom Business imeonyesha dhamira kuwa ni mbia katika kuleta teknolojia zinazorahisisha biashara na kuwezesha kuhimili ushindani, huku wakiongeza ufanisi na  kuwezesha kujenga mtandao katika uendeshaji.
“Sisi ni kampuni ya huduma za simu inayotoa huduma kupitia ubunifu wa kiteknolojia zinazoweza kurahisisha biashara, shughuli za viwanda na kuleta mabadiliko “alimazia kusema Bw. Hendi.

Loading...

No comments: