Vyakula Bora kwa Tumbo na Afya Njema! - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, March 2, 2019

Vyakula Bora kwa Tumbo na Afya Njema!


Ikiwa unasumbuliwa mara kwa mara na maradhi ya tumbo kama tumbo kujaa gesi na kuunguruma au kutopata choo, ni ukweli usiopingika unatamani sana kuondokana na maradhi hayo. Unaweza kuwa kama wengine wengi waliojaribu aina mbalimbali ya virutubisho vinavyouzwa kwenye maduka ya vyakula na dawa vyenye nembo zinazodai kutatua matatizo ya tumbo, wametumia na bado unasumbuliwa tu.

Mabadiliko madogo ya vyakula unavyokula yanaweza kukusaidia kukabiliana na maradhi ya tumbo na kuwa na afya njema. Aina tatu muhimu za vyakula muhimu kwa tumbo lako, inahusisha vyakula vyenye nyuzinyuzi kama mboga za majani, probiotiki na pribiotiki.
Vyakula vyenye nyuzi husaidia kudhibiti mwendo ambao vyakula hutembea kwenye utumbo.Probiotiki kwenye vyakula ni vimelea vyenye faida vilivyotengenezwa kwa kuchachusha (fermentation). Ni vimelea ambavyo vinaweza kupambana na vimelea vingine vinavyosababisha maradhi ambayo wakati mwingine vinaweza kuingia kwenye vyakula tunavyokula. Pribiotiki ni vyakula muhimu kwa probiotiki kuwa katika hali nzuri na kustawi zaidi.

Tafiti zimeonyesha vyakula vyenye vimelea vyenye faida kama maziwa mgando (mtindi) husaidia kusawazisha viwango vya bakteria ndani ya tumbo na kuondoa tatizo la kutopata choo. Vimelea hivyo vinaweza kuboresha kinga ya mwili kiujumla kwa kupambana na vimelea vya maradhi vilivyoingia tumboni pamoja na chakula ulichokula.

Vyanzo vikuu vya vyakula vyote vitatu ni pamoja na nafaka na maziwa. Kwa kula vyakula kama nafaka isiyokobolewa mfano ugali wa dona hufanya mtu kupata virutubisho vyote vilivyopo kwenye vyakula hivyo. Vyakula vinavyotokana na nafaka isiyokobolewa huwa na virutubisho vinavyosaidia mfumo wa umeng'enyaji chakula na afya yote kiujumla.Mwanamke anahitaji gramu 25 za vyakula vya nyuzinyuzi kila siku sawa na vikombe vidogo viwili vya maharage na mwanaume gramu 38 sawa na vikombe vidogo vitatu vya maharage. Kula zaidi ya mahitaji ya mwili kwa siku huweza kusababisha tumbo kuuma na kujaa gesi. Na kwasababu vyakula vya nyuzinyuzi hufanya kazi vizuri kwenye uwepo wa maji hivyo ni vyema kunywa maji ya kutosha muda wote wa siku.

Unaweza kufikia kirahisi mahitaji ya siku ya vyakula vya nyuzinyuzi kwa kuchanganya mboga jamii ya kunde kama maharage, dengu na kunde ambapo utahitaji kikombe kidogo kimoja kwa siku. Ikiwa una wasiwasi wa tumbo kujaa gesi inashauriwa kuloweka maharage kwa muda mrefu kabla ya kuyapika hiyo inaweza kupunguza kiwango cha gesi. Tafiti zinadai vile unatumia jamii ya kunde mara kwa mara ndivyo unavyopunguza kiwango cha gesi baada ya kula kwa maana tumbo huzoea.
Loading...

No comments: