WAKALA WA BALE AWEKA WAZI KUWA BALE HAENDI POPOTE PALE. - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, March 4, 2019

WAKALA WA BALE AWEKA WAZI KUWA BALE HAENDI POPOTE PALE.


Wakala wa Gareth Bale, Jonathan Barnett amesema kwamba mteja wake haendi kokote majira haya ya kiangazi lakini amewatupia lawama kubwa mashabiki wa Real Madrid.

Bale alizomewa na mashabiki wa Real Madrid pindi alipokuwa anatoka baada ya kudumu uwanjani kwa saa moja katika mechi dhidi ya Barcelona na Barnett amesema,"Kizazi cha mashabiki wa Real Madrid wataongelea kuhusu magoli ya Gareth kwa miaka kadhaa ijayo, kiukweli waone aibu ."

"Gareth anastahili heshima sana, jinsi mashabiki wa Real wanavyomfanyia ni ukosefu mkubwa sana wa heshima." 

Unadhani BALE akibaki Madrid anaweza kuonyesha makali yake au ni wakati wa yeye kwenda timu nyingine akapate changamoto nyingine. 
Loading...

No comments: