WAKATI MAJONZI YA RUGE HAYAJAISHA, MTANGAZAJI EPHRAIM KIBONDE AFARIKI DUNIA


Wakati bado familia, wafanyakazi wa Clouds Media Group na watanzania kwa ujumla tukiwa katika majonzi yakuondokewa na kipenzi cha watu, aliyekuwa mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media bwana Ruge Mutahaba, leo mapema hii habari zimetufikia kuwa aliyekuwa mtangazaji wa redio ya clouds fm hasa katika kipindi cha jahazi, Ephraim Kibonde amefariki dunia. 

Kupitia mtandao wa Twitter, mfanyakazi mwenzake Millard Ayo alipost na kusema "Mkuu wa mkoa wa Mwanza amethibitisha kwamba Mtangazaji wa Clouds Fm Ephraim Kibonde amefariki akiwa Mwanza, alianza kusumbuliwa na presha toka Bukoba kwenye msiba wa Ruge Mutahaba na kuhamishiwa Mwanza. #RIPKibonde" 

Kibonde alifiwa na mkewe mnamo mwishoni mwa mwaka jana na wiki iliyopita alimpost instagram huku akionesha kumkumbuka sana na kuumia kwa kifo cha mwenza wake huyo. 

Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya marehemu na pole nyingi ziende kwa familia ya Kibonde, wafanyakazi wa Clouds, marafiki na ndugu wote. 

Ephraim Kibonde enzi za uhai wake.


Post a Comment

0 Comments