WAMILIKI WA MANCHESTER CITY WANAFIKIRIA KUNUNUA TIMU NCHINI INDIA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, March 5, 2019

WAMILIKI WA MANCHESTER CITY WANAFIKIRIA KUNUNUA TIMU NCHINI INDIA


Imeripotiwa kuwa kampuni ya CITY FOOTBALL GROUP (CFG) ambayo inamiliki timu nyingi za michezo ikiwemo mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Uingereza, Manchester City wanafikiria kununua klabu ya mpira wa miguu nchini India kulingana na maelezo ya mkurugenzi wao Ferran Soriano. 

Kampuni hiyo kwa sasa inamiliki klabu kama New York City, Melbourne City, Manchester City ambayo imeonyesha kuwaletea mafanikio makubwa mpaka sasa pamoja na klabu zingine 4 ulimwenguni hapa. 

CFG pia wiki mbili tu zilizopita imenunua klabu ya SICHUAN JIUNIU ya china na sasa Soriano anasema wana mpango wa kuwekeza nchini India. 

Mkurugenzi mkuu wa Manchester City, Ferran Soriano
CFG ilianzishwa mwaka 2013 wakati timu ya New York City inanunuliwa na kuwa klabu ya pili kumilikiwa nao baada ya Manchester City. Ferran alidokeza kuwa kampuni hiyo inaweza kuongeza japo timu 2 au 3 za ziada na kwa sasa wanajaribu kufikiria kuwekeza nchini India. 
Loading...

No comments: