WANANCHI WA MSUMBIJI HATARINI KUKUMBWA NA KIMBUNGA HATARI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, March 16, 2019

WANANCHI WA MSUMBIJI HATARINI KUKUMBWA NA KIMBUNGA HATARI


Watu wanaoishi katika mji mkuu wa Msumbiji Maputo wameonywa kutokea kwa hali mbaya zaidi kutokana na kimbunga kikali.

Tufani iliyopewa jina la Idai, ambayo inabeba upepo wenye kasi ya kilomita 225 kwa saa itasababisha kimbunga kikali karibu na bandari ya Beira, mji wenye watu wapatao laki tano.
Mvua kubwa iliyonyesha nchini humo tayari imesababisha vifo vya watu 100 nchini Msumbiji na Malawi.

Beira ni mji wa nne kwa ukubwa nchini Msumbiji ambapo bandari yake iko katika mdomo wa mto Pungwe ambao umekwenda mpaka Zimbabwe.

Kitengo cha hali ya hewa cha Ufaransa ambacho kinashughulikia maeneo yanayodhibitiwa na Ufaransa katika eneo la Bahari ya Hindi kimeonya kuwa hali inaweza kuwa mbaya kutokana na maji kujaa mengi. 

Loading...

No comments: