Wanawake wengi hupenda wanaume wenye sifa hizi katika mahusiano ya kimapenzKatika safari yeyote ile ya mahusiano ya kimapenzi baina ya mwanamke na mwanaume yapo mambo mbalimbali yanapaswa kuzingatiwa ili kufanya mahusiano hayo yaweze kudumu, na miongoni mwa vitu vitakavyofanya mapenzi yadumu ni pamoja na kuwako kwa tabia ambazo zitakazowasaidia wapenzi hao waweze kuelewana.

Muungwana blog inakusogezea kwako tabia  zifuatazo ambazo wanawake wengi huzipendelea kutoka kwa wanaume zao ili waweze kudumu katika mahusiano ya kimapenzi :

Mwanamke humpenda mwanaume mwenye kujali na kuheshimu hisia za mwanamke.
Endapo utapata mwanaume mwenye kujali hisia zako za kimapenzi basi huyo ndiye mwanaume sahihi kwako, kwani hukuna kitu kizuri kama kuwa kwenye mahusiano na mtu anajali hisia zako na si kuziumiza.

Mwanaume mwenye akili za utafutaji wa maisha.
Katika ulimwengu wa mahusiano hakuna kitu kizuri kama kumpata mwanaume mwenye akili timamu za utafutaji na upambanaji wa maisha, hivyo kila wakati ewe mdada mwenye uchu wa ndoa kama utaka mwanaume sahihi kwako basi unatakiwa kuhakimisha unashughurika na mwanaume mwenye akili za utafutaji wa kimaisha na si vinginevyo.

Mwenye kujua mwanamke anataka nini haswa.
Unajua wapo wanaume ambao ni mahili sana wa kusema fulani nakupenda sana, ila ukweli ukiwachunguza watu hao huongozwa na tamaa tu, kwani wapo wanaume wachache sana ambao wanaojua kiundani kuwa mwanamke anataka nini haswa. Ngoja nikuibie siri ewe mwanaume unayesmoama makala haya, mwanamke anahitaji kuona unamjali ili awe na amani ya moyo.

Mwanaume ambaye anathamimi na kumjali msichana.
Jambo ambalo mwanamke anahitaji kutoka kwa mpenzi wake ni upendo na kujaliwa, mwanamke mwenye hisia thabiti anapenda kuona mwanaume wake anamjali na kumpenda kila wakati na hivyo kila wakati wanaume wanashuriwa kuwajali wapenzi wako kadri wawezavyo.

Mwanaume mwenye kukujulia hali kila wakati.
Asikwambie mtu mapenzi ya kweli ni uzao utokanao na mawasiliano thabiti baina ya wapenzi hao, hivyo mwanamke hupenda mawasilino mazuri kutoka kwa mume wake, hivyo ewe mwanaume kila wakati unatakiwa kumjali mwenza wako kwa kuongeza mawasiliano kwani hii ndiyo njia pekee ya kuonesha ujali hatiamaye muweze kusumu katika mahussssianao yenu.

Mwanaume mwenye kujali ndugu na jamaa na marafiki wako wa karibu.
Kila mwanamke anapenda kuona mbali na kuonesha upendo wako kwake pia napenda kuona unajali watu ambao wanamzunguka pia. Watu kama wazazi, ndugu na marafiki unatakiwa kuonesha upendo wako kwao pia hii itawafanya watu hao waone kuwa unafaa sana.

Asante kwa kusoma makala haya kutoka hapa Muungwana blog, tukutakie siku njema na utekelezaji mwema.

Na. Benson Chonya. 

Post a Comment

0 Comments