WATANZANIA WATAKAOWAKILISHA VIJANA ECOSOC MAREKANI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, March 30, 2019

WATANZANIA WATAKAOWAKILISHA VIJANA ECOSOC MAREKANI


Kila mwaka Umoja wa Mataifa hufanya mkutano mkuu wa mwaka ujulikanao kama  'ECOSOC  Youth Forum (Economic and Social Council) au kwa kiswahili 'Mkutano wa Vijana wa Uchumi na Jamii (ECOSOC) ambapo linalenga kuwaleta vijana karibu kutoka pande mbalimbali za dunia kujadili Malengo ya Maendeleo Endelevu au SDGs. Mwaka huu baraza hili litafanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) nchini Marekani, mjii mkuu wa New York kuanzia tarehe 8-9 mwezi wa nne. Dhima kuu ya mwaka huu inalenga kujadili hatua zilizopigwa na nchi mbali mbali kwenye kutekeleza SDGs kuanzia malengo haya yalipozinduliwa rasmi mwaka 2015 na Umoja wa Mataifa. “Empowered, Included and Equal”,   Pia itaangalia malengo makuu matano ya maendeleo endelevu katika maeneo ya elimu bora (SDG4), kazi zenye staha na ukuaji wa uchumi (SDG8), usawa (SDG10), hali ya hewa (SDG13), amani, haki na taasisi imara (SDG16), na ushirikiano wa malengo (SDG17)

Mkutano huu utawapa fursa vijana kutoka mabara mbalimbali kujadili kwa kina Agenda ya Malengo ya Maendeleo Endelevu, Addis Ababa Action pamoja na Paris Agreement. Pia itakuwa ni sehemu ya kuwakilisha nchi ambazo zinafanya mchakato wa hiari wa kukusanya maoni kuhusu utekelezaji wa SDGs. Mwaka huu Tanzania imeingia kwenye mchakato huu kwa mara ya kwanza ambapo tumeona mashirika mbali mbali, serikali, watu binafsi na azaki za kiraia zikifanya mikutano mbalimbali hapa nchini.

Kutoka Tanzania mwaka huu vijana wa tatu wataiwakilisha Tanzania kwenye mkutano huo ambao ni Adam Anthony (OSIEA), Hussein Melele (Mulika Tanzania) na Jolson Masaki (YUNA Tanzania). Hawa ndio vijana watakaoiwakilisha nchi yetu pamoja na vijana watanzania kwenye hili huu mkutano. Hii ni sehemu ya ule mkutano mkuu wa 'High-level Political Forum 2019'.
Tunatarajia mengi kutoka kwao na uwakilishi wa nchi na changamoto zinazowakabili vijana kwa ujumla. Mkutano huu utafuatiwa na mkutano mwingine mkuu ambao utawasilisha maoni ya nchi kuhusu malengo ya maendeleo endelevu ambao utafanyika pia New York mwezi wa saba.

Loading...

No comments: