Waziri Atembeza Bakuli Yanga Apata Milioni - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, March 14, 2019

Waziri Atembeza Bakuli Yanga Apata Milioni


Waziri Atembeza Bakuli Yanga Apata Milioni
NAIBU Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde, ambaye ni mwanachama wa Yanga, juzi aliunga mkono kampeni ya kocha wa timu hiyo, Mwinyi Zahera kwa kuanzisha rasmi kampeni ya kutembeza bakuli kwa wanachama wa timu hiyo waishio mikoa ya kanda ya kati kwa kukusanya zaidi ya shilingi milioni moja.Mavunde ambaye amechaguliwa na Yanga kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uhamasishaji, juzi alianzisha rasmi kampeni hiyo ya kuzungusha bakuli.Akizungumza wakati wa kampeni hiyo, Mavunde alisema kuwa pamoja na kuhakikisha anatekeleza sawasawa jukumu hilo, pia ameutaka uongozi wa Yanga kuwatambua wanachama wote wa mikoani kwa kupitia kadi zao za uanachama ili waweze kuhakikisha wanalipa michango yao ya kila mwezi ili kuinua njia ya mapato sahihi.“Nimeamua kuanza kutekeleza wajibu wangu kama mwenyekiti wa hamasa lengo ni kuona tunapata fedha nyingi zitakazoisaidia timu yetu kujinusuru katika wakati huu mgumu tunaopitia pamoja na kwamba nimeanza kwa kukusanya zaidi ya milioni moja kutoka kwa wadau wetu.“Mbali na hivyo pia tupo katika mbio za kugombea ubingwa na tayari tupo nafasi ya kwanza tukiongoza ligi, hivyo nia yetu tunajitahidi kufanya hivi ili tuweze kuwapa nguvu wachezaji wetu na kocha wetu ambaye anajitoa sana kwa ajili yetu ili aweze kutwaa kombe,” alisema Mavunde. 
Loading...

No comments: