YALIYOJIRI EUROPA: 'GOLIATI ARSENAL' AANGUSHWA NA 'DAUDI RENNES', CHELSEA, NAPOLI, VALENCIA, VILLAREAL ZAANZA VYEMA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, March 8, 2019

YALIYOJIRI EUROPA: 'GOLIATI ARSENAL' AANGUSHWA NA 'DAUDI RENNES', CHELSEA, NAPOLI, VALENCIA, VILLAREAL ZAANZA VYEMA


Klabu ya Arsenal ya jijini London jana imewatia aibu mashabiki zake mara baada ya kupokea kichapo kitakatifu cha 3-1 kutoka kwa timu ya Rennes ya Ufaransa katika mchezo wa raundi ya 16 bora ya ligi ya Europa. 

Walikuwa ni Arsenal walioanzisha mapigano kwa kupata goli la mapema mnamo dakika ya 3 tu kupitia kwa Mnigeria Alex Iwobi. Dakika ya 42, ambayo ni dakika moja baada ya beki wa Arsenal Sokratis kupewa kadi nyekundu, Benjamin Bourigeaud akaisawazishia Rennes na matokeo mpaka mapumziko kuwa 1-1. 

Kipindi cha pili ndipo Goliati Arsenal wanaojiamini mno walipofundishwa mpira na vijana wa Rennes ambao wana hali mbaya katika ligi yao wakiwa wameachwa zaidi ya point 30 na vinara PSG. Dakika ya 65 beki wa Arsenal Nacho Monreal anajifunga na kufanya matokeo kuwa 2-1. Na wakati Arsenal wakidhani mechi itaisha hivyo, Mchezaji Ismaila Sarr akapachika msumari wa mwisho mnamo dakika ya 88 na mpaka mpira unaisha Rennes walishinda 3-1. 

Katika mechi zingine, Chelsea akiwa nyumbani Stanford Bridge akamfunga Dynamo Kyiv 3-0, Napoli pia akiwa nyumbani kamchapa Redbull 3-0, Valencia akiwa nyumbani kashinda 2-1 dhidi ya Fc Krasnodar, Villareal akiwa ugenini akamchapa Zenit 3-1, Sevilla akatoka droo ya 2-2 na Slavia praha, Intermillan akatoka droo tasa ugenini ya 0-0 dhidi ya Eintracht, Dinamo Zagreb akamchapa Benfica 1-0. 

Mechi za marudiano zitachezwa wiki ijayo tarehe 14 na 15 mwezi March na ndizo zitakazoamua nani aingie hatua ya robo fainali na nani anatolewa. 
Loading...

No comments: