Zitto mgonjwa, kesi yake yakwama, hakimu atoa neno - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, March 11, 2019

Zitto mgonjwa, kesi yake yakwama, hakimu atoa neno


 Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe ameshindwa kufika mahakamani kwa sababu zilizoelezwa kuwa ni mgonjwa.
Zitto anakabiliwa na mashtaka matatu katika kesi ya uchochezi, inayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Taarifa ya ugonjwa wa Zitto, zimetolewa leo Jumatatu Machi 11, 2019 na wakili wake, Steven Mwakibolwa, baada ya upande wa mashtaka kuieleza Mahakama hiyo kuwa hawamuoni mshtakiwa mahakamani hapo.
Wakili wa Serikali, Wankyo Simon amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakamani hiyo, Huruma Shaidi, kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kuanza usikilizwaji wa ushahidi, lakini mshtakiwa hayupo mahakamani hapo na upande wa mashtaka hawana  taarifa zake.
“Upande wa mashtaka tayari tunaye shahidi mmoja ambaye ni ASP Shamila Mkoma na tupo tayari kuendelea na ushahidi, lakini kwa bahati mbaya hatumuoni mshtakiwa mahakamani hapa, wakili wake yupo hapa atatuambia alipo mshtakiwa,"amedai Simon.
Simon baada ya kueleza hayo, Wakili Mwakibolwa, anayemtetea Zitto amedai mteja wake ni mgonjwa na leo, ameshindwa kufika mahakamani kusikiliza kesi yake.
"Nimepewa taarifa asubuhi hii kuwa Zitto ni mgonjwa, lakini amekuja shemeji yake mahakamani hapo kutoa taarifa hivyo, ataieleza mahakama juu ya afya ya Zitto," amedai Mwakibolwa.


Loading...

No comments: