AJIRA 44,000 KUTOLEWA NA SERIKALI

BUNGE limeelezwa kuwa katika mwaka wa fedha 2019/20, serikali itaajiri watumishi wapya 44,807 wa kada mbalimbali. Miongoni mwa kada zitakazoajiri watumishi wengi ni Elimu (13,526), Afya (9,467), Jeshi la Polisi (3,725).

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora), George Mkuchika
Kada zingine ni Kilimo, Mifugo na Uvuvi (2,141), Magereza (685), Jeshi la Zimamoto na Uhamiaji (500), Hospitali za mashirika ya dini na hiari (1,262) na pia watumishi 13,002 wa kada nyingine wakiwamo wahadhiri wa vyuo vikuu vya umma.

Kauli hiyo ilitolewa bungeni jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora), George Mkuchika, alipokuwa akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2019/2020.

Alisema mbali na kuajiri, pia watumishi 290,625 watapandishwa vyeo kulingana na maelekezo yatakayotolewa.

Post a Comment

0 Comments