AKOTHEE AWEKA WAZI MIPANGO YAKE YA KUHAMIA KWENYE MUZIKI WA INJILI MUDA SI MREFU

Akothee Gospel

Baada ya siku chache kuweka wazi kuwa ameokoka, msanii wa Kenya mwanamama Akothee ana mpango wa kuacha kabisa muziki wa kawaida (kidunia) na kuanza kufanya muziki wa Injili. 

Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Akothee alikaririwa akisema; "Tumesahau kuwasifia na kuwapongeza wasanii wetu na tunawakumbatia sana wasanii wa nje. Utakuta wimbo ni mbovu kabisa lakini unakuwa Hit hapa Kenya." alisema Akothee 

"Ninawapongeza wasanii wote wa injili kwa sababu kanisani hakuna yoyote ambaye anahitaji kukuonesha ushirikiano. Hauihitaji kujipongeza mwenyewe kwasababu kanisa kila siku limejaa. Ndio maana nataka kuhamia huko (kanisani) kwa sababu ni rahisi kwangu. Kila mtu anamhitaji Yesu, au sio?" Alimalizia mwanadada huyo

Wakati hayo yakitokea wadau mbalimbali wamekuwa na maoni tofauti na Akothee huku wengi wakisema kuwa wasanii wengi hukimbilia muziki wa injili pale tu wanapoona wamechuja na hawawezi kuhimili ushindani wa soko la muziki wa kawaida. 

Wewe unaonaje? 

Post a Comment

0 Comments