ALAN SHEARER HAONI MAN CITY WAKICHUKUA MAKOMBE MANNE MSIMU HUU KAMA WENGI WANAVYOTABIRI


Nguli wa soka nchini Uingereza Alan Shearer ameamua kwenda kinyume kidogo na watu wengi ambao wanaipa matumaini na kuona uwezekano wa klabu ya Manchester City kuchukua makombe manne msimu huu.  

Shearer anasema kuwa haoni Manchester City ikichukua makombe manne msimu huu hasa kombe la ligi ya mabingwa Ulaya ambapo kwa yeye anaona uwepo wa klabu ya FC Barcelona na nyota wake Lionel Messi ndio utakaoharibu ndoto hizo. 

"Barcelona na Lionel Messi ndio sababu kubwa inayofanya nisifikirie kama Manchester City watatwaa mataji manne." alisema Shearer ambaye amekuwa akichambua michezo mingi ya Ligi kuu ya Uingereza. 

Alan Shearer amesema kwamba anaamini Man City watatwaa taji la FA lakini kukamilisha mataji manne kuna kisiki mbele yao. 

Manchester City wameshashinda kombe la ligi (CARABAO), wapo katika fainali ya EMIRATES FA CUP ambayo watacheza na Watford tarehe 18 MAY, wapo katika mbio za ubingwa wa EPL wakipambana na Liverpool na pia wapo hatua ya Robo fainali katika ligi ya mabingwa barani Ulaya. 

Je unadhani Manchester City wataweza kuchukua makombe manne msimu huu? 

Post a Comment

0 Comments