AMIN ATOBOA KUHUSU YEYE NA LINAH

Staa wa Bongo Fleva, Amini amefungukia ukaribu wake na msanii wakike Linah Sanga kufatia picha zao kuzua gumzo kwenye mtandao wa Instagram.Ukaribu waliouonesha kwenye picha za wawili hao ambao waliwahi kuwa wapenzi na kuachana ziliwafanya wengi kuhusisha ukaribu huo na kurudi kwa penzi kati ya wawili hao hasa baada ya kila mmoja kuachana na mzazi mwenzake. 

Hata hivyo Amin amefunguka na kueleza kuwa wao wanafanya kazi na kuhusu mapenzi imebaki historia kwao.

Akiongea na MCL Digital, Amin amesema kuwa walikuwa kwenye maandalizi ya kazi yao iitwayo “Nimenasa”.

Amesema wimbo ambao ni maalumu kwa wapenzi utaingia mtaani leo na mashabiki wao wategemee kupata ladha nzuri.

“Nimeamua kufanya kazi hii na Lina kwa sababu ni miongoni mwa wasanii wa kike ambao wako vizuri, ana kipaji na muda wote yuko tayari kwa kazi.”

Kuhusu ukimya wake wa muda mrefu Amin ameeleza kuwa unatokana na shughuli mbalimbali lakini anaamini mashabiki wake wapo.

Amesema:”Kuna msanii na mwanamuziki, najivunia kuwa mwanamuziki na mashabiki wanajua muziki mzuri, tumelelewa katika misingi hiyo,”

Amin pia amesema kwamba daima atamkumbuka Ruge kwa kuwa alimlea katika malezi ya kuwa mwanamuziki anayejitambua na kujua thamani yake si kuishi kwa kiki. 

Post a Comment

0 Comments