AZINDUKA KUTOKA KITANDANI BAADA YA KUZIMIA KWA MIAKA 27 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, April 24, 2019

AZINDUKA KUTOKA KITANDANI BAADA YA KUZIMIA KWA MIAKA 27

Mwanamke mmoja kutoka Umoja wa falme za kiarabu(UAE) aliumia sana katika ajali ya gari ilitokea mwaka 1991 na kupoteza fahamu lakini sasa amestaajabisha wengi baada ya kuamka kutoka kwenye koma iliyomchukua miaka 27 akiwa amepona.


Munira Abdulla,alipata ajali akiwa na umri wa miaka 32 na kupata jeraha katika ubongo . Munira alipa ajali kwa kugongwa na basi wakati akiwa anaelekea kumchukua mtoto wake shuleni.

Mtoto wake Omar Webair, alikuwa na umri wa miaka minne wakati yeye na mama yake walipopata ajali. Katika ajali hiyo Omar ambaye alikuwa ameketi katika kiti cha nyuma hakujeruhiwa hata kidogo na alikutwa akiwa amekumbatiwa na mama yake.
Bi.Abdulla alijeruhiwa vibaya lakini mwaka jana akiwa hospital moja Ujerumani alianza kurudisha fahamu.

Omar ameweka wazi kuhusu ajali walioipata na kuelezea utaratibu wa matibabu ya mama yake yaliyochukua miaka mingi.

Omar aliongeza kusema kuwa sababu kubwa ambayo imemfanya asimulie mkasa uliomkuta mama yangu ni kutaka kuwaambia watu kuacha kukata tamaa kwa watu wanaowapenda na mtu akifikia hatua hiyo haimaanishi kuwa amekufa.

Mama mkwe wa Munira ndio alikuwa dereva " Mama yangu alikuwa amekaa na mimi katika kiti cha nyuma , na alipoona tunakaribia kupata ajali, alinikumbatia ili kuniokoa katika ajali hiyo."

Katika ajali hiyo Omar hakuumia bali alibaki na jeraha dogo kichwani lakini mama yake ambaye aliumia alichelewa kupata matibabu kwa saa kadhaa.
Bi. Abdalla alifikishwa hospital baada ya muda wa saa kadhaa kupita na baadae alihamishiwa mji wa London huku walisema kuwa amepoteza fahamu lakini akiwa ana uwezo wa kuhisi maumivu.

Baada ya muda lirudishwa katika mji wa Al Ain katika umoja wa falme za kiarabu ambako alikuwa akiishi na mtoto wake Omar, na kuendelea kuzunguka katika vituo mbalimbali vya afya kulingana na bima aliyokuwa nayo.

Alikuwa anakula kwa mrija na kumfanya aendelee kuishi na mara kwa mara alifanyiwa mazoezi na vipimo vya viungo ili kuhakikisha kuwa misuli yake haidhoofiki kwa kuwa alikuwa atembei.
Loading...

No comments: