Batuli Atoboa Anachotamani Kwa Manara - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, April 29, 2019

Batuli Atoboa Anachotamani Kwa Manara

STAA wa Bongo movie, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’, amefunguka kitu anachokitamani kutoka kwa msemaji wa Simba ni pamoja na siku moja kufanya maamuzi magumu na kuchukua kadi ya kuwa mwanachama hai wa Yanga.
Batuli, ambaye ni shabiki mkubwa wa Yanga, amesema licha ya mapenzi makubwa aliyonayo kwa msemaji huyo wa Simba, lakini anatamani kuona akifanya maamuzi hayo na kujiunga na Yanga.

“Kitu ambacho ukiniuliza natamani nini zaidi kwa Manara ambaye ni rafiki yangu wa karibu, nitakwambia natamani ajiunge Yanga, najua si rahisi na hata kwa wengine wataona kuna ugumu kidogo, lakini naamini maamuzi kama hayo ni ya kawaida sana na huenda akafikiria ombi langu,” alisema Batuli.
Loading...

No comments: