BENIN KUFANYA UCHAGUZI BILA WAGOMBEA WA UPINZANI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, April 29, 2019

BENIN KUFANYA UCHAGUZI BILA WAGOMBEA WA UPINZANI

Wananchi wa Benin wanashiriki uchaguzi wa wabunge wapya bila wagombea wa upinzani.

Uchaguzi Benin

Tume ya uchaguzi mwezi uliyopita iliviidhinisha vyama viwili vya kisiasa vinavyodaiwa kumuunga mkono rais Patrice Talon kushiriki uchaguzi huo baada ya kufikia masharti yaliyowekwa.

Sheria mpya ya uchaguzi ilivitaka vyama kulipa ada ya dola 424,000 ili viruhusiwe kushiriki uchaguzi huo.

Huduma ya intaneti imedhibitiwa huku mitandao ya kijamii na huduma ya kutuma na kupokea ujumbe mfupi zikifungwa katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

Wapiga kura milioni tano wamesajiliwa kushiriki zoezi hilo katika taifa hilo linalojivunia kuwa na utawala thabiti wa kidemokrasia.


HATUA INAYOWEZA KUZUA GHASIA: 
Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wamekosoa hatua ya kuzuiliwa kwa maandamano ya amani na kukamtwa kwa wanaharakati wa upinzani wanaolalamikia hatua ya upinzani kufungiwa uchaguzi huo.

"kuongezeka kwa visa vya kukamatwa na kuzuiliwa kwa wapinzani huenda kukazua ghasia nchini humo," François Patuel, kutoka shirika la Amnesty International, alisema katika taarifa yake.

"Kupiga marufuku maandamano ya amani na kuwakamata na kuwazuilia wale wanaopinga hatua ya upinzani kufungiwa nje ya uchaguzi kutazua hali ya mtafaruku."

Wiki iliyopita, vikosi vya usalama viliwarushia vitoza machozi marais wa zamani wa nchi hiyo- Nicéphore Soglo na Thomas Boni Yayi walipokua wakiwahutubia waandamanaji kuhusu suala la uchaguzi katika mji wa Cotonou.

Rais Talon, aliingia madarakani mwaka 2016. Mfumo wa siasa ya vyama vingi ilibuniwa miaka mitano iliyopita nchini Benin, na uchaguzi wa kwanza chini ya mfumo huo ulifanyika miaka ya 1990, ambapo vyama 20 viligombania viti 83 vya ubunge, kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari la AFP.

Rais Talon, ambaye ni mfanyibiashara wa zamani aliyejulikana kama "mfalme wa pamba", aliingia madarakani mwaka 2016.

Anasema marekebisho ya sheria ya uchaguzi yanalenga kuleta pamoja mamia ya vyama vya upinzani vilivyo na falsafa aina moja kwa lengo la kuimarisha mfumo wa siasa ya vyama vingi.

Bw Talon pia alitia saini sheria ya kuwazuia wafanyikazi wa afya na wafanyikazi wengine wa serikali kugoma kwa zaidi ya siku 10.

Mamia ya waendesha piki piki waijitokeza kusikiliza houba ya marais wawili wa zamani waliyokua wakishinikiza kucheleweshwa kwa uchaguzi

Wanahabari wanasema watu wengi walitarajia kuwa uchaguzi huo utaahirishwa ili kuvipatia vyama vya upinzani muda wa kufikia masharti mapya ya uchaguzi.

Lakini katika hotuba yake kwa taifa Aprili 11, rais Talon alisema kuwa hana mamlaka ya kuingilia machakato wa uchaguzi. 
Loading...

No comments: