BIERBER MATATANI TENA KWA KUMGONGA RIPOTA LOS ANGELES - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, April 17, 2019

BIERBER MATATANI TENA KWA KUMGONGA RIPOTA LOS ANGELES


Unalikumbuka tukio la msanii na staa Justin Bieber kumngonga na gari mpiga picha mmoja wakati akitoka kanisani mjini Los Angeles mwaka 2017? I hope utakuwa unakumbuka. Sasa za chinichini zinasema kuwa mpiga picha huyo amesogea mahakamani.

Mtandao wa The Blast umeripoti kuwa, William Wilson (mpiga picha huyo) amemshtaki Justin Bieber kwa uzembe uliopelekea ajali ile. William amedai kuwa alikuwa amesimama upande wa waenda kwa miguu na Bieber ameipeleka gari lake moja kwa moja na kumgonga. 

Hata hivyo mwimbaji huyo alijitetea na aliwaambia waandishi waliokuwepo eneo hilo kuwa hakufanya makusudi bali ni kutokana na kuyumba kiafya. 

Bierber alionesha ushirikiano hadi gari la wagonjwa lilipofika na kumchukua ripota huyo, na taarifa za polisi wa Beverly Hills zilisema kuwa Justin Bieber alishirikiana nao vyema. Hivyo hakufunguliwa shauri lolote lile. 

Kwanini huyu jamaa anafungua mashtaka sasa? Au kafulia? Hebu tupe comment zako pia. 
Loading...

No comments: