BOBI WINE AWEKWA KIZUIZINI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, April 23, 2019

BOBI WINE AWEKWA KIZUIZINI

Polisi na jeshi nchini Uganda jana jioni walizingira nyumba ya Mbunge wa Kyadondo mashariki Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine, saa kadhaa baada ya kutangaza mpango wake wa kutembea hadi polisi katika maandamano ya umma kupinga ukatili dhidi ya tamasha zake za muziki na wanasiasa wa upinzani.


Aliwataka waganda wote wenye hasira kuungana nae katika mapambano dhidi ya ukosefu wa haki.

Bobi Wine aliwekwa katika kizuizi cha nyumbani katika kile ambacho polisi walisema ilikwa ni hatua ya kumzuwia mwanasiasa huyo wa upinzani kufanya mikutano iliyo kinyume cha sheria.

Saa kadhaa awali , Bobi Wine alikuwa ametangaza mpango wa kufanya maandamano ya umma kote nchini kupinga hatua ya polisi kuendelea kuweka vikwazo dhidi ya tamasha zake za mziki na ukatili dhidi ya wanasiasa wa upinzani.

"Nilitaka kuiambia dunia kile kinachofuatia na hicho ndicho polisi hawakutaka kukisikia.

Tumetumia njia zote za kisheria polisi wasitusimamishe kuzuwia maonyesho yangu na kuwatesa wapinzani lakini wameshindwa kuelewa. Ninatoa wito wa kuwepo kwa mbinu nyingine za kisheria ambazo ni kupinga ," Bobi Wine alivieleza vyombo vya habari kwenye makazi yake ya Kasangati.

BBC swahili
Loading...

No comments: