CHUCHU HANSY AFUNGUKIA VIDEO YA RAY KIGOSI NA MWANAMKE MWINGINE

Staa mrembo kutoka Bongo Movie, Chuchu Hansy ‘Kichuna’ amesema alijisikia vibaya kuona video ya mzazi mwenzie Ray Kigosi, staa wa Bongo Movie akiwa na mwanamke mwigine.

Leo akiwa kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM, Chuchu alisema;

"Zile video zake mimi niliziona kama watu wengine walivyoziona, nilijisikia vibaya lakini nitafanyaje yote kheri, sikumuuliza maana nina vitu vingi vya kufanya kwa sasa na kama nikikaa na kufatilia mapenzi zaidi mambo mengine naweza nisifanye maana mapenzi yanacost sana”

Video iliyosambaa mtandaoni inamuonyesha Ray Kigosi akiwa na mwanamke mwingine ndani ya gari wakiongea maneno  yanayoashiria ukaribu wakutilia mashaka.

Akizungumzia kuhusu mahusiano yake na Ray Kigosi,  Chuchu alisema ana historia ya kudumu muda mrefu kwenye mahusiano, yeye na Ray wanatimiza miaka kumi mwezi wa tano mwaka huu 2019.

 “Huwa nina historia ya kudumu muda mrefu kwenye mahusiano, mimi na Ray ikifika mwezi wa tano tunatimiza miaka kumi kwenye mahusiano”.

Post a Comment

0 Comments