DAVID BECKHAM AZUNGUMZA KISWAHILI

Mcheza mpira maarufu wa zamani wa taifa ya Uingereza David Beckham hajulikana kuwa na ujuzi wa kujua lugha nyingi lakini anaongoza kampeni dhidi ya malaria ambapo anaonekana akizungumza lugha tisa. 

Anaonekana katika filamu fupi akizungumzia vita dhidi ya Malaria na kupitia kamera na teknolojia ya tarakilishi anazungumza kiswahili, Kinyarwanda, Kiarabu, na kiarabu miongoni mwa lugha nyengine.

Mdomo wake na uso unalingana na matamshi yake lakini sauti zinazosikika zinatoka kwa manusura wa ugonjwa wa malaria.

Waandalizi wanatumai kwamba watu wengine duniani wataingia na kuongeza sauti zao. Sauti zitakazopatikana zitatumika kuwashinikiza viongozi duniani huku wakiandaa kufanya maamuzi kuhusu hazina ya kukabiliana na Ukimwi, TB na Malaria.

Post a Comment

0 Comments