DROO YA AFCON 2019: TANZANIA KUKUTANA NA KENYA, ALGERIA NA SENEGAL

Droo ya upangaji wa makundi kwa mashindano ya Mataifa ya Afrika 2019, Misri umemalizika hivi punde jijini Cairo Misri.

Timu ya Tanzania, Taifa Stars imepangwa katika Kundi C la mashindano hayo lenye timu za Kenya, Algeria na Senegal.
Ukiondoa kundi hilo la Stars, Kundi A linaundwa na wenyeji Misri, Zimbabwe, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huku kundi B likiwa na timu za Nigeria, Guinea, Burundi na Madagscar na kundi D linaundwa na timu za Namibia, Afrika Kusini, Ivory Coast na Morocco.

Tunisia wameangukia kundi E pamoja na timu za Angola, Mali na Mauritania wakati Kundi F lina timu za Cameroon, Guinea Bissau, Ghana na Benin.

Michuano hiyo itafanyika nchini Misri kuanzia Juni 21 hadi Julai 19 mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments