UZINDUZI WA EAST AFRICA GOT TALENT WAFANYIKA JIJINI NAIROBI

Got Talent ni maalumu kwa ajili ya watu kuonyesha vipaji vyao walivyonavyo, mf. Kuimba, kucheza, mazingaumbwe, vipaji vya kula, kulia au kucheka. Kwa yoyote mwenye kipaji chochote anapata nafasi ya kuonyesha.Got Talent ipo katika Mabara na nchi mbalimbali mfano “Amerca Got Tallent” , Britain Got Talent, Asia Got Talent, Spain Got Talent na nyingine nyingi. Sasa ni zamu ya Afrika Mashariki – EAGOT.

Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga ni mmoja watu mashuhuri waliokuwepo kwenye uzinduzi huo, amesema kuwa ni kama ndoto imetimia kwani walipambana kuipata EAGT.

‘’Ni kama ndoto imetimia, nimepambana kuhakikisha tunaipata hii EAGT, tunasherehekea miaka 20 ya Clouds Media na sababu kubwa ya kuendelea kusheherekea ni kuendelea kuwapa watu burudani na wengi kutimiza ndoto zao’’ Alisema Joseph Kusaga.

Aidha alisema Clouds Media msingi wake ni kufungulia watu dunia, na itabakia hivyo na Clouds itakuwa ni kwa ajili ya watu, na East Afrika imebarikiwa vipaji, yeye na team yake itahakikisha EAGT inatumika kunufaisha East Afrika haswa vijana

East Africa Got Talent itahusisha Kenya, Rwanda, Uganda na TanzaniaUzinduzi huo wa East Africa Got Talent umefanyika Movenpick Hotel Mjini Nairobi na umehudhuriwa na Mawaziri mbalimbali kutoka Serekali ya Kenya, Wasanii, Wakuu wa mashirika na makampuni mbali mbali.

Post a Comment

0 Comments