FAMILIA YA MAREHEMU PRINCE RODGERS NELSON YATANGAZA KUFILISIKA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, April 29, 2019

FAMILIA YA MAREHEMU PRINCE RODGERS NELSON YATANGAZA KUFILISIKA

Rodgers Nelson

Siku 8 zimepita tangu itimie miaka mitatu ya kifo cha nguli wa muziki wa Pop Prince Rogers Nelson ambaye alitajwa kufariki kwa kuzidisha utumizi wa dawa za kupooza maumivu maarufu kama Fentanyl.

Sasa familia yake imeibuka na kudai itakuwa imefilisika hadi kufikia mwaka ujao, 2020. Dada wa Prince, Sharon Nelson amesema kutoelewana kati ya familia na benki ya Comerica Bank & Trust kunapelekea hilo kutokea.

Sharon amesema familia imekuwa ikipambana kupata pesa za marehemu Prince kutoka kwenye benki hiyo ambapo kwa muda sasa hawajafanikiwa licha ya kuendelea kupoteza pesa nyingi kwa ajili ya kuendesha kesi na kuajiri wanasheria. Mpaka sasa wametumia zaidi ya Tsh. Bilioni 6.

Loading...

No comments: