FEKIR AKARIBISHA OFA KUTOKA VILABU VINAVYOMTAKA KATIKA DIRISHA LIJALO LA USAJILI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, April 2, 2019

FEKIR AKARIBISHA OFA KUTOKA VILABU VINAVYOMTAKA KATIKA DIRISHA LIJALO LA USAJILI


Nahodha wa klabu ya Olympique Lyon, Nabil Fekir ambaye majira ya kiangazi yaliyopita alikaribia kutua Liverpool, ameliambia jarida la Telefoot kwamba anaweka mlango wazi kuhusu majira ya kiangazi ya mwaka huu kwa timu yoyote inayomtaka. 

Katika mahojiano hayo Fekir alisema, "Liverpool? Ni sehemu ya maisha ya soka ya mchezaji, lakini pia inakufanya uwe imara na inabidi usonge mbele. Sijui nini nitafanya majira ya kiangazi."

"Lakini kama nilivyosema, najisikia vizuri sana hapa Lyon, Rais wa klabu ananiamini sana. Hiyo ni vizuri sana. Kwahiyo nitaangalia kama nitasaini mkataba mpya au la." 

Loading...

No comments: