FLORA BADO NI MKE WANGU-H.BABA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, April 5, 2019

FLORA BADO NI MKE WANGU-H.BABA

Msanii wa Bongo Fleva, Hamisi Ramadhani ‘H.Baba’ amefungukia swala la kuachana na Mke wake Flora Mvungi staa wa Bongo Movie na kusema kwamba hajampa talaka mkwe wake kama inavyodaiwa. 

H.Baba na mkewe Flora
 
Akiongea na EATV.TV, H.Baba amesema kwamba kitu anachojua ni kwamba Flora bado ni mkewe kwani yeye ndiye aliyeoa, hivyo kama ni talaka yeye ndiye mwenye kuitoa lakini kamwe hajafanya hivyo. 

H.Baba ameendelea kusema kwamba kauli ya Flora kuwa ndoa ya wawili hao imekufa sio kweli, na kama Flora ndiye aliyeoa basi atoe talaka ili kuvunja ndoa hiyo. 

 “Maisha yangu ya muziki hayaingiliani na familia yangu na watoto, sikumuoa instagram, kwa sababu unapozungumza ili watu wakusikie, ili u-trend sio kitu cha busara kwa sababu unaongea uongo, mimi ninachojiua ni mtu ambaye sijampa talaka, na mtu ambaye hatuna ugomvi, mimi niko busy na baishara zangu". 

 “Kwa mfano mimi ningekuwa nimefungwa miaka mitano angeniacha!?. Na yeye ni mke wangu, mimi nimemuoa kwa dini na sheria za Kiislam, kwa hiyo kama ataomba talaka atanitafutia mke, atanitolea mahali atanipa huyo mke nitatoa talaka, mimi ninachojua yeye ni mke wangu. 

Wanaosema nan'gang'ania, mwanaume anang'ang'ania ndoa!?. Mimi naangalia watoto wangu, lakini hajaniomba na tupo vizuri, yule ni mke na atabakia kuwa mke”, amesema H.Baba. 

Familia ya H.Babba
Hivi karibuni kumekuwa na mvutano kati ya wawili hao kudai kuwa wameachana. Taarifa ambayo imetolewa na mwenyewe mke wa H Baba, Flora Mvungi huku H Baba akiendelea kukanusha kuwa hajamtaliki mkewe na bado wako vizuri.
Loading...

No comments: