'GOAL POACHER' SERGIO AGUERO KUIKOSA MECHI YA MAN CITY NA CARDIFF LEO - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, April 3, 2019

'GOAL POACHER' SERGIO AGUERO KUIKOSA MECHI YA MAN CITY NA CARDIFF LEO


Kocha wa klabu ya ManchesterCity, Pep Guardiola amethibitisha kwamba straika wake Sergio Kun Aguero ataikosa mechi ya leo jumatano dhidi ya Cardiff City ya Ligi kuu ya Uingereza (EPL). 

Kun Aguero alitolewa nje kwenye mechi ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Fulham siku ya Jumamosi na Guardiola amethibitisha kwamba Mu'Argentina' huyo hayupo fiti kucheza leo Jumatano. 

"Hakufanya mazoezi kwenye siku mbili zilizopita, kesho hatoweza kucheza. Ni matumaini yetu Jumamosi ijayo au Jumanne tutaona mabadiliko yake." Alisema kocha huyo wa mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Uingereza. 

Katika kukazia hilo, kocha Guardiola amethibitisha kwamba straika kinda mbrazil, Gabriel Jesus ataanza kikosini katika mechi dhidi ya Cardiff itakayopigwa katika dimba la Etihad leo. 

Loading...

No comments: