GRIEZMANN YUPO TAYARI KUPUNGUZA MSHAHARA WAKE ILI ATUE BARCA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, April 2, 2019

GRIEZMANN YUPO TAYARI KUPUNGUZA MSHAHARA WAKE ILI ATUE BARCA


Staa wa klabu ya Atletico Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa, Antoine Griezmann yupo tayari kupunguza kiasi cha Pauni milioni 6 kwenye mshahara wake ili kujiunga na mabingwa watetezi wa Laliga FC Barcelona kwa mujibu wa taarifa kutoka vyombo vya habari vya nchini Hispania. 

Mfaransa huyo alikataa kujiunga na FC Barcelona majira ya kiangazi yaliyopita na kusaini mkataba mpya na mrefu wa kubaki 'Wanda Metropolitano' mpaka ifikapo mwaka 2023. 

Lakini jarida la Mundo Deportivo limedai kwamba Griezmann anajutia uamuzi huo na ameanza kuwa na hofu kwamba huenda akastaafu bila taji la UEFA Champions League. 

Loading...

No comments: