HABARI MBAYA KWA DORTMUND NA MOROCCO, HAKIMI KUWA NJE MPAKA MWISHO WA MSIMU - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, April 2, 2019

HABARI MBAYA KWA DORTMUND NA MOROCCO, HAKIMI KUWA NJE MPAKA MWISHO WA MSIMU


Ni majanga kwa klabu ya Borussia Dortmund na Morocco ndivyo unavyoweza kusema kutokana na habari ya kuwa beki wa pembeni wa Dortmund na timu ya taifa ya Morocco, Achraf Hakimi atakuwa nje ya dimba kwa muda wote uliobaki wa msimu huu baada ya kuumia mifupa ya vidole vya mguu kwenye mechi ya ushindi wa klabu yake 2-0 dhidi ya Wolfsburg juzi. 

Leo hii vinara wa Bundesliga wamethibitisha kupitia ukurasa wao rasmi wa Twitter kwamba Hakimi aliye kwa mkopo kutoka Real Madrid atarejea Madrid kwa ajili ya kufanyiwa Operesheni na hatocheza tena msimu huu. 

Hakimi mwenye umri wa miaka 20 anatarajiwa kucheza mashindano yake ya kwanza ya AFCON akiwa na Morocco miezi mitatu kuanzia sasa lakini kucheza kwake nchini Misri mwezi Juni kumeingiwa na mashaka makubwa baada ya majanga haya kumtokea. 

Kukosekana kwa Hakimi kutafungua mlango kwa beki wa kushoto wa Schalke, Hamza Mendy kuanza kuchezeshwa. 
Loading...

No comments: