Hali ni Mbaya:Mafuliko Nchini Msumbiji, Watu 700,000 Hatarini - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, April 29, 2019

Hali ni Mbaya:Mafuliko Nchini Msumbiji, Watu 700,000 Hatarini

Hali kaskazini mwa Msumbiji ni mbaya kuliko ilivyodhaniwa, msemaji wa Umoja wa mataifa ameeleza, siku chache baada ya kimbunga Kenneth kutuwa nchini humo.Kimbunga hicho kilituwa siku ya Alhamisi kwa upepo mkali wenye kasi ya 220km/h (140mph) kilichoviangamiza vijiji.

Takriban watu 700,000 sasa wanadhaniwa kuwa katika hatari katika eneo hilo wakati mvua kubwa ikiendelea kunyesha.

Pemba, mji mkubwa wa jimbo la Cabo Delgado kumeshuhudiwa mvua yenye kina cha mita mbili na mafuriko.

Msemaji katika ofisi ya uratibu wa masuala ya kibinaadamu (Ocha) Saviano Abreu ameeleza kwamba hali ni mbaya katika miji ya Macomia na Quissanga, akiongeza kwamba kuna wasiwasi pia kwa kisiwa kisichoweza kufikiwa cha Ibo.

Mawimbi ya hadi mita 4 yanatarajiwa, na mashirika ya misaada yanahofia kwamba mvua itazidi kunyesha.

Inadhaniwa kwamba watu 400,000 wanaishi Pemba , na mvua kubwa imesababisha watu wengi kuwa katika hatari.

Kuna wasiwasi unaotokana na maporomoko ya ardhi katika mtaa wa Mahate mjini humo, maafisa wa Ocha katika eneo hilo wanasema, na katika mtaa wa Natite, nyumba zimeanza kuporomoka.

Shirika la mpango wa chakula duniani linaarifiwa kuanza kutoa misaada kwa watu waliokwama, lakini barabara zilizoharibika zimesababisha shughuli zisitishwe katika maeneo yaliotengwa sana.

Takriban watu watano wamefariki kutokana na kimbunga hicho na takriban nyumba 35000 zimeharibika vibaya au kubomoka kabisa, maafisa wa kitaifa wanasema.


BBC Swahili
Loading...

No comments: