HIVI HAPA VILABU VINAVYOONGOZA KWA KUWA NA WASTANI MZURI WA KUJAZA VIWANJA VYAO KWA MIAKA 5 ILIYOPITA.

Uwanja wa FC Barcelona, CAMP NOU


Hakuna ubishi kuwa klabu ya Simba ndio inayoongoza kwa kujaza uwanja wa taifa hapa nchini, uwanja ambao ndio mkubwa kuliko vingine vyote wenye uwezo wa kupokea watu 60,000. Na pongezi ziwaendee Haji Manara na timu yake nzima ya habari na mahusiano na umma. wanafanya kazi njema sana. 

Sasa kwa mujibu wa The CIES Football Observatory, klabu ya Borussia Dortmund ndio inayoongoza kwa kuwa na wastani wa maudhurio ya juu katika kipindi cha miaka mitano iliyopita yaani kutoka  mwaka 2013 hadi 2018. 

The CIES Football Observatory wamefanya tathimini katika nchi 42 na kugundua kwamba uwanja wa klabu ya Manchester United, Old Trafford una wastani wa kuingiza watu 75,218 huku Dortmund wakiwa kinara kwa kufikisha wastani wa watu 80,230 kwa mechi moja. 

Ifuatayo ni List ambayo The CIES wameitoa: 

1. Borussia Dortmund – Average attendance between 2013-2018 = 80,230

2. Manchester United – Average attendance between 2013-2018 = 75,218

3. Barcelona – Average attendance between 2013-2018 = 74,876

4. Bayern Munich – Average attendance between 2013-2018 = 73,781

5. Real Madrid – Average attendance between 2013-2018 = 69,822

6. Schalke – Average attendance between 2013-2018 = 61,328

7. Arsenal – Average attendance between 2013-2018 = 59,793

8. Hamburg – Average attendance between 2013-2018 = 52,349

9. Stuttgart – Average attendance between 2013-2018 = 52,012

10. Atlanta United – Average attendance between 2013-2018 = 51,547 

Je klabu yako unayoishabikia ipo katika orodha hii? 

Post a Comment

0 Comments