HOJA KUICHANGIA YANGA YAKWAMA BUNGENI

Leo asubuhi Aprili 5, 2019, baada ya Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kuitambulisha kamati ya kuhamasisha kuichangia Yanga iliyoalikwa kutembelea Bunge, Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keissy  aliomba mwongozo akitaka wabunge kuichangia klabu ya Yanga kwa kutatwa sehemu ya posho zao kuichangia Klabu ya Yanga ya Dar es Salaam.Kessy amesema kutokana na uwepo wa kamati hiyo, ni vyema likapitishwa kapu bungeni ili wabunge nakupendejkeza wabunge  wakatwe Sh. 100,000 kila mmoja katika posho yao ya leo ili kuichangia klabu hiyo inayokabiliwa na ukata.

Dk Tulia alilihoji Bunge kuhusu hoja hiyo ya Keissy, “Wabunge walio tayari kuchangia waseme ndio na wasio tayari waseme sio.”

Kutokana na wabunge wengi kusema sio, Dk Tulia amesema waliokataa hoja hiyo ni wengi zaidi, hivyo haijapitishwa.

Post a Comment

0 Comments