HUU NDIYO MJENGO WA MBOSSO! - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, April 1, 2019

HUU NDIYO MJENGO WA MBOSSO!

Msanii wa Bongo Fleva kutoka lebo ya WCB, Mbosso amewaonyesha mashabiki wake mjengo anaoumiliki kwasasa ukiwa ni zao la mafanikio yake kimuziki.


Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram, Mbosso alitupia pich ahiyo hapo juu na kuandika haya akianza na kwa kumshukuru Mungu.

“Mwenyezi Mungu ni Mkubwa sana na anasiri kubwa sana katika kila ya mja wake (..Asante Mola wangu..)..., huenda hiki kikawa kidogo sana kwa wengine ila kwangu Mimi nikikubwa sana , tena sana kwa sababu sikuwa na uwezo nacho awali, ila tu Mapenzi yenu na Sapot yenu kwangu mmenifanya leo hii na Mimi niwe na kwangu”-Aliandika.

 "Eti Mbosso na Mimi leo nina kwangu 😭.." , "Acha niseme asanteni sana kwa upendo wenu, asanteni kwa Kuokoa kipaji changu na kuamua kunisapot tangu siku ya kwanza hadi kufiki leo hii .." Hiki ni kidogo mulichoweza kunifanya nimiliki leo hii kijana wenu.. "Mungu awabariki sana na awafungulie milango yenu ya rizki kwa upana zaidi " ili mupate nguvu ya kuendelea kunisapot Kijana wenu " inshaalla"🙏”- Alimaziliza.

Kabla ya kuwachini ya WCB Mbosso alikuwa moja ya wasanii vijana waliokuwa wakiunda kundi la Yamoto Band ambalo lilitamba sana kwenye ulimwengu wa Bongo Fleva kabla ya kusabaratika miaka ya hivi karibuni.
Loading...

No comments: