JACQUELINE AFUNGUKA JINSI ALIVYOKUTANA NA DR.MENGI

Miss Tanzania (2000), muimbaji wazamani wa Bongo Fleva  na mlimiki wa kampuni ya Amorette Ltd, Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi ambaye ni mke wa Dr Reginald Mengi mmiliki wa kampuni ya IPP Media, ameleza jinsi wawili hao alivyokutana na sasa kuwa mke na mume.
Mr &Mrs Mengi


Leo mchana akizungumza kwenye kipindi cha XXL  cha Clouds FM, Jacqueline amesema kwa mara ya kwanza walikutana na Dr. Mengi ikiuwa kwenye ndege wakati akienda London uingereza, ikiwa ni mara yake ya kwanza kuonana naye uso kwa uso.

"Nilikutana na mume wangu wakati naenda London, ilikuwa kwenye ndege na tulizungumza maongezi ya kawaida na kuanzia hapo ndiyo tukaanza mawasiliano, kabla ya hapo sikuwahi kumuona popote"

Akizingumzia swala la pesa katika mahusiano, Jacqueline alisema pesa sio kila kitu katika maisha  ya mahusiano.

“Pesa sio kila kitu kwenye mahusiano maana Pesa inaweza kuwepo na kesho isiwepo naamini kikubwa ni unapokuwa kwenye mahusiano tafuta mtu ambaye ni rafiki kwako na mimi nasema kila siku Mume wangu ni rafiki yangu”. Jacqueline alisema.

Kuhusu tofauti ya kiumri kati yake na Dr Mengi, Jacqueline alieza kuwa huo ni mtazamo tu wa watu kwani mtu anaweza kuwa tofati na jinsi anavyoonekana kwa nje.

“Usimhukumu mtu kwa mtu unavyomuona, mume wangu ukimuona na ukimjua ni tofauti, Mimi na Mume wangu tumekuwa kwenye mahusiano karibia miaka 9 na ili muanze mahusiano ya kweli lazima muanze kama marafiki" – Jacqueline alieleza.Mapema wiki hii Jacqueline na mume wake Dr. Mengi wamesherekea miaka nne ya ndoa yao, wakiwa na familia ya watoto wawili.

Post a Comment

0 Comments