JOKATE ATOA NENO KWA ‘KONKI LIQUID’ - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, April 1, 2019

JOKATE ATOA NENO KWA ‘KONKI LIQUID’

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo ametoa shukrani zake kwa msanii Peter Molel maarufu kama Konki Liquid 'Pierre' kwa uwepo wake kwenye hafla ya Tokomeza Zero Kisarawe iliyofanyika kwenye ukumbi wa mlimani city jijini Dar siku ya jumamosi .


 
 
Jokate ambaye  muandaaji wa shughuli hiyo Jokate ametumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram kushukuru watu mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo akiwemo Konki Liquid.

“Hakuna maneno muhimu na machache katika ustawi wa maisha ya binadamu kama tafadhali, asante na samahani. Katika dhifa niliyoiandaa jana, nilialika watu wengi, wanasiasa, taasisi za kiserikali, mabalozi, wafanyabiashara, wajasiriamali, wasanii, wadau wa burudani n.k,” amesema.

“Na kwangu mimi na wilaya nzima ya Kisarawe wote waliofika jana ni muhimu sana sana kwangu na kwetu.”

Katika kuonyesha sababu iliyomfanya kiongozi huyo kuandika ujumbe huo, amesema kipekee anamshukuru Konki Liquid @officialpiere_liquid kwani wapo watu maarufu aliowaalika lakini hawakuweza kufika.

“Ila wewe ulichukua muda wako kuhamamisha na kufika na zaidi ya hapo ukatoa mchango wa Sh100,000! Hukuja kuuza sura tu! Nasema asante sana. Wana Kisarawe tunakupenda na tunakukaribisha kuwekeza Kisarawe uanzishe hata mgahawa tutakusaidia kupata eneo.

“Lakini pia nimesikia ni mtengenezaji mzuri sana wa furniture. Hii shule tunayoenda kujenga inahitaji madawati naomba tufanye kazi na wewe katika hii fursa. Tuangalie namna japo kidogo tukuwezeshe.

Tunasema karibu Kisarawe ukae. Kisarawe Kunogile. Tunasema samahani kwa kukwazika lakini zaidi Asante kwa kushiriki kwenye #TokomezaZeroKisarawe #ElimuItabakiKuwaJuuKileleni #KisaraweMpya Ubarikiwe!” Aliandika.

Maneo hayo ya Jokate yameonekana kuwatia moyo masanii Pierre na mashabiki wake kufuatia maneno ya  mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda  aliyoyazungumza kwenye hafla hiyo akivitaka vyombo vya habari kuwaibua watu wanaofanya mambo ya maana huku akimtolea mfano Konki Liquid kuwa ni mtu wa ajabu aliyepewa umaarufu bila sababu.

WAZIRI KIGWANGALLA AFUNGUKA SAKATA LA PIERRE


Loading...

No comments: