KAJALA AWAUMA SIKIO MASHABIKI ZAKE

Staa wa mrembo Bongo Movie, Kajala Masanja  amsema si lazima kuonekana kwenye kazi nyingi ili kipaji chake kiendelee kwa juu.Akizungumza jijini Dar es Salaam, mwanadada huyo amesema anaweza kuwa kimywa kwa muda, lakini bado uwezo wake wa uigizaji utaendeleakuwa palepale.

Alisema anatambua mashabiki wana hamu ya kumuona katika filamu akiendeleza kipaji chake,hivyo waendelee kusubiri muda wowote kazi zake mpya zitaweza kuingia sokoni.

“Mashabiki waendelee kusubiri kazi zangu zinaendelea kuandaliwa,kila kitu kitakapokamilika zitaingia sokoni,watarajie mambo mazuri Zaidi,” alisema Kajala.

Kajala ni muigizaji na mmiliki wa Kajala Entertainment,kampuni inayoshighulisha na maswala ya burudani ususani uandaaji na utengenezaji wa filamu.

Post a Comment

0 Comments