KISIKI VAN DIJK AMPIGIA KURA STERLING MCHEZAJI BORA WA MWAKA EPL


Beki kisiki wa Liverpool Virgil van Dijk amempigia kura mchezaji wa Manchester City Raheem Sterling kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Ligi kuu ya Uingereza na amesema kwamba kuna baadhi ya wachezaji wa City angeweza kuwapigia kura pia. 

"Nimefanya ambacho nimefikiria na nimefikiria kwamba anastahili. Amekuwa na msimu bora sana na ningeweza kumpigia kura Bernardo Silva na baadhi ya wachezaji wengine wa City." Alisema Van Dijk. 

"Lakini nimeamua kuwa mkweli. Nafikiri kiwango chake kimepanda sana kama mchezaji. Tutaona kama atashinda."alimalizia Van Dijk

Kanuni za tuzo za mchezaji bora wa mwaka wa EPL (PFA) zinasema kuwa mchezaji hutakiwi kuwapigia kura wachezaji wa kikosi cha timu yako. Ndio maana unaona Van Dijk kampigia Raheem Sterling. 

Post a Comment

0 Comments