KOCHA McCLAREN ATIMULIWA NA QUEENS PARK RANGERS


Klabu ya Queens Park Rangers (QPR) wamemfukuza kazi kocha wao Steve McClaren baada ya kuwa na mfululizo wa matokeo mabovu tokea alipoajiriwa na waingereza hao. 

McClaren katika msimu huu ameweza kushinda mechi moja tu katika mtiririko wa mechi 15 za ligi ya Championship Uingereza, kitu amabacho kinawatia wasiwasi mabosi wa klabu hiyo huku malengo yao ya kurudi ligi kuu ya Uingereza yakizidi kuyoyoma miaka nenda miaka rudi. 

Steve McClaren mwenye umri wa miaka 57 aliwahi kuwa kocha wa Timu ya Taifa ya Uingereza kati ya Agosti 2006 mpaka Novemba 2007 na aliajiriwa na QPR mnamo mwezi Mei mwaka jana 2018. 

Post a Comment

0 Comments