KOCHA WA MAN UNITED: TUTAPINDUA MATOKEO HISPANIA

Kocha  wa Manchester United ,Ole Gunnar Solskjaer atalazimika kufanya kazi ya ziada kupata matokeo mazuri katika mchezo ujao wa robo fainali ya pili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati timu hiyo itakapokuwa ugenini kuivaa Barcelona kwenye Uwanja wa Nou Camp.
 


Kipigo cha bao 1-0 ilichopata jana usiku kinamuweka kocha huyo katika nafasi ndogo ya kusonga mbele ingawa amedai ana timu imara inayoweza kufanya maajabu katika mchezo huo wa wiki ijao.

Solskjaer alisema Man United ina nafasi ya kufunga bao katika mchezo huo kwa kuwa ana kikosi imara

Mshambuliaji huyo wa zamani wa timu hiyo ana amini kama aliweza kupindua matokeo katika mchezo dhidi ya Paris Saint Germain PSG hakuna ana nafasi pia ya kufanya hivyo Hispania.

“Tumepata mafanikio makubw akutokana na historia ya Barcelona. Bado tuko katika ushindani, itakuwa mechi ngumu lakini tuliwahi kufanya hivyo hapo nyuma,” alisema nguli huyo wa Norway.

Beki wa kushoto Luke Shaw alijifunga dakika ya 12 kutokana na mpira wa kichwa uliopigwa na Luiz Suarez aliyeunganisha krosi ya Lionel Messi.

“Kimsingi lilikuwa bao bora kutokana na kazi nzuri ya Messi na Suarez. Messi ni mchezaji wa aina yake,” alisema Solskajaer.

Katika mechi nyingine Ajax Amsterdam ikiwa nyumbani Uholanzi ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Juventus

Post a Comment

0 Comments