KUMBE ARIANA GRANDE NA BEYONCE WALILIPWA SAWA BWANA!!!Baada ya taarifa kutoka kwamba Beyonce na Ariana Grande wamelipwa tofauti na Grande amemzidi Beyonce kwenye kutumbuiza kwenye tamasha la Coachella 2018 na 2019, imedaiwa kuwa hakuna ukweli wa hilo.

Mtandao wa The Blast umeripoti kuwa taarifa hiyo ilinukuliwa vibaya na usahihi wake ni kuwa wote walilipwa ($8 million) Tsh. Bilioni 18, lakini mfumo wa malipo ndio uliotofautiana kati yao. 

Ariana Grande alilipwa pesa zote kutumbuiza wikendi mbili huku Bey alilipwa kwa 'instalment' yaani kwa wikendi moja alilipwa ($4 million) na nyingine akamaliziwa wikendi ya mwisho. 

Nadhani hapo watakuwa wameeleweka. 

Post a Comment

0 Comments