KUNA HILI JIPYA LINAPIKIKA KATI YA INTERMILLAN NA MAURO ICARDI


Inter Milan wanajiandaa kumpa ofa ya mkataba mpya Straika wao Mauro Icardi ambao utakuwa na kipengele cha kupunguza thamani yake kwenye mkataba kutoka Pauni Milioni 100 mpaka Pauni Milioni 50 kwa vilabu vya nje ya Italia tu. 

Muargentina huyo hakucheza kwenye kikosi cha Inter Milan tangu mwezi Februari baada ya kunyang'anywa kitambaa cha unahodha na klabu hiyo kufuatia kutoelewana kwao. 

Icardi na Inter Millan wamekuwa katika migogoro na kutoelewana kwa muda sasa na kila mmoja anavuta kamba upande wake ingawa hii inaonekana kumuumiza zaidi Mauro Icardi. 

Hii inasemekana kuwa ni njama ya kumuuza mchezaji huyo tena kwa bei chee kwa timu za nje ya Italia. Je Icardi atakubali au atawaletea ngumu akigundua njama hiyo? 

Post a Comment

0 Comments